Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Morocco, Ismael Saibari, amekamilisha rasmi uhamisho wa kujiunga na Bayern Munich akitokea PSV Eindhoven, baada ya pande zote kukamilisha taratibu zote za usajili.
Kwa mujibu wa taarifa, Bayern Munich imefikia makubaliano na PSV Eindhoven ya kumsajili Saibari kwa ada ya euro milioni 55, huku nyaraka zote za uhamisho zikiwa zimesainiwa Kilichobaki ni klabu hiyo kumtangaza rasmi kama mchezaji wake mpya.
Saibari anajiunga na Bayern Munich baada ya kuonyesha kiwango kizuri akiwa PSV Eindhoven, jambo lililovutia klabu hiyo ya Bundesliga kuhitaji huduma yake katika dirisha hili la usajili.
Mbali na kiwango chake akiwa ngazi ya klabu, Saibari pia amekuwa na mchango kwa timu ya taifa ya Morocco katika Kombe la Dunia 2026, hadi sasa, mshambuliaji huyo amefunga mabao matatu katika michezo minne aliyocheza, akisaidia Morocco kufuzu hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.
Uhamisho huo ni maandalizi ya Bayern Munich kuelekea msimu mpya, huku Saibari akitarajiwa kuanza safari mpya ya soka nchini Ujerumani mara baada ya kutangazwa rasmi na klabu hiyo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment