Shalulile atua Yanga akiwa na mabao matatu msimu wa 2025/26

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa mshambuliaji , Peter Shalulile baada ya mkataba wake na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2025/26.

Shalulile ni raia wa Namibia mwenye umri wa miaka 32 anayecheza nafasi ya mshambuliaji wa kati ambaye Pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Namibia.

Mshambuliaji huyo alianza soka la kulipwa akiwa Tura Magic ya Namibia kabla ya kuhamia Highlands Park ya Afrika Kusini mwaka 2015. Mwaka 2020 alijiunga na Mamelodi Sundowns, ambako alicheza hadi kumalizika kwa mkataba wake.

Katika msimu wa 2025/26, Shalulile amecheza michezo 13 ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini na kufunga mabao matatu, huku Katika mashindano yote ya msimu huo, alicheza michezo 31 na kufunga mabao sita.

Yanga imepata mshambuliaji mwenye uzoefu wa kucheza ligi ya kubwa na mashindano ya CAF, wakati ambao ikijiandaa kwa msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments