Sababu za Olise kuposti picha zisizo na ubora kombe la Dunia zawekwa wazi

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kilichoonekana kama jambo la kawaida kwenye machapisho ya mshambuliaji wa Ufaransa, Michael Olise, wakati wa Kombe la Dunia, sasa kimeibua simulizi tofauti baada ya kufahamika sababu ya picha zake zilizoonekana kuwa na ubora wa chini(low quality).

Tangu kuanza kwa kombe la Dunia, Olise amekuwa akichapisha picha zilizokuwa na ubora wa chini kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii. Hatua hiyo iliwafanya mashabiki wengi kuamini kuwa ilikuwa sehemu ya mtindo wake au ujumbe uliohusu mustakabali wake, hasa baada ya kufuta machapisho yote kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Taarifa zinaeleza kuwa mpiga picha wake binafsi alishindwa kuingia Marekani kwa ajili ya Kombe la Dunia kutokana na changamoto za VISA.


Badala ya kumtafuta mpiga picha mwingine, Olise aliamua kuendelea kufanya kazi na mtu ambaye amekuwa akinasa matukio ya safari yake ya soka kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mpiga picha huyo aliendelea kupiga picha za Olise akiwa nyumbani kupitia matangazo ya televisheni, huku Olise akiendelea kuzichapisha katika mitandao ya kijamii wakati wote wa mashindano.


Uamuzi huo umeelezwa kuwa ulikuwa njia ya kuendelea kushirikiana na mpiga picha wake licha ya kutokuwepo uwanjani, jambo lililobadili mtazamo wa wengi kuhusu picha ambazo awali zilionekana kuwa za kawaida.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com



0/Post a Comment/Comments