Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
KLABU ya Al Ahly itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) msimu wa 2026/27 baada ya Shirikisho la Soka la Misri (EFA) kuthibitisha ushiriki wa timu hiyo kufuatia uamuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kukataa ombi la kuongeza idadi ya timu za Misri katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Awali, EFA iliwasilisha ombi kwa CAF likitaka kuruhusiwa kuingiza timu zaidi ya kiwango kinachoruhusiwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Endapo ombi hilo lingekubaliwa, Al Ahly ingeendelea kushiriki mashindano hayo licha ya kutomaliza katika nafasi mbili za juu katika ligi Yao
Hata hivyo, CAF ililitupilia mbali ombi hilo na kubaki na utaratibu wake wa kawaida wa uwakilishi wa vilabu katika mashindano ya ngazi ya klabu barani Afrika.
Kutokana na uamuzi huo, EFA imethibitisha kuwa Al Ahly itawakilisha Misri katika Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao badala ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Wakati huo huo, shirikisho hilo limetangaza kuwa leseni ya klabu ya Zamalek imeidhinishwa, hatua inayoiruhusu kushiriki mashindano ya CAF msimu wa 2026/27.
0767815473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment