Rais wa Argentina agoma kuhudhuria fainali ya kombe la Dunia

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Rais wa Argentina, Javier Milei, amesema hatahudhuria fainali ya Kombe la Dunia itakayowakutanisha mabingwa watetezi Argentina na Hispania Julai 19, 2026, akieleza kuwa uamuzi huo unatokana na imani na utaratibu alioufuata tangu mwanzo wa mashindano.

Milei amesema hatafanya mabadiliko yoyote katika namna alivyokuwa akifuatilia safari ya timu ya taifa ya Argentina, akiamini kuwa kubadili utaratibu huo kuelekea mchezo wa mwisho kunaweza kuathiri bahati ya timu yake.

Kiongozi huyo alifafanua kuwa katika michezo yote ya Argentina kwenye mashindano hayo amekuwa akizitazama akiwa nyumbani, jambo ambalo amesema atafanya hivyo hivyo hata kwenye mchezo wa fainali unaosubiriwa na mashabiki duniani.

Kutokana na msimamo huo, Milei amesema hataenda uwanjani kushuhudia pambano hilo ana kwa ana, badala yake atalifuatilia akiwa nyumbani kama alivyofanya katika michezo yote iliyopita.

Argentina wataingia uwanjani kusaka taji la nne katika mashindano hayo , huku Spain wakisaka taji lao la pili katika mashindano hayo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments