PAZIA LA LIGI KUU BARA KUFUNGULIWA AGOSTI 12

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Ligi kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2026/27 utaanza rasmi kwa mchezo wa ngao ya jamii utakao wakutanisha bingwa wa ligi kuu na bingwa  kombe la shirikisho Yanga dhidi ya Simba siku ya agosti 12, 2026 huku ligi hiyo ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi siku ya Agosti 14, 2026 na kutamatika Mei 16, 2027.

Awali mchezo wa ngao ya jamii ulikuwa ukihusisha timu nne ambazo zilianza hatua ya nusu fainali na hatimaye fainali ili kumpata bingwa , kwa sasa mchezo utachezwa mmoja kutokana na ratiba kuwa ngumu kufuatia kuwepo na mashindano ya kufuzu Afcon na Afcon yenyewe ambapo Tanzania ni nchi mwenyeji kwa ushirikianao wa Kenya na Uganda.

Kutajwa kwa Tarehe ya kuanza kwa mashindano ni taa ya tahadhari kwa vilabu nchini kuhakikisha kuwa vinaanza maandalizi mapema ili kutengeneza timu imara na kuepuka matokeo mabovu kwenye msimu mpya wa mashindano.

0767815473,

lugembetimothy01@gmail.com.

 

 

0/Post a Comment/Comments