OLISE AMFUNIKA PELE PASI ZA MABAO KOMBE LA DUNIA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa Ufaransa, Michael Olise, ameweka rekodi kwenye Kombe la Dunia 2026 baada ya kufikisha pasi Saba za mabao (asisti) na kuvunja rekodi ya nguli wa Brazil, Pele aliekuwa na assist sita zilizodumu tangu mwaka 1970.

Olise aliifikia na kuvunja rekodi hiyo katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu dhidi ya England, ambapo alitoa pasi mbili za mabao na kufikisha jumla ya asisti saba katika mashindano hayo.

Kabla ya mafanikio hayo, Pele alikuwa akishikilia rekodi ya asisti nyingi zaidi katika toleo moja la Kombe la Dunia kwa zaidi ya miaka 50, tangu alipoisaidia Brazil kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 1970.

Kwa kufikisha idadi hiyo ya asisti, Olise amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Kombe la Dunia kutoa pasi saba za mabao ndani ya toleo moja la mashindano, hatua iliyo mfanya kuwa ndiye mfalme wa pasi za mabao kwenye mashindano hayo.

Hivyo, mchango wa mchezaji huyo umeisaidia Ufaransa kumaliza nafasi ya nne kwenye mashindano hayo japo imekuwa kinyume Cha matarajio ya Wengi ambapo awali ilionekana ndiyo namba Moja kwenye kinyanganyiro Cha ubingwa ila safari imetamatika wakiwa hawajatimiza lengo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.





0/Post a Comment/Comments