Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mfungaji wa muda wote wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr, ametangaza kumaliza safari yake ya kulitumikia taifa hilo kisoka baada ya kueleza kuwa amefikia mwisho wa kipindi chake akiwa na kikosi cha timu ya taifa.
Neymar ametoa mchango wake kwa Brazil na anaamini umefika wakati wa kuondoka ili kutoa nafasi kwa kizazi kingine cha wachezaji kuendelea na jukumu la kuiwakilisha nchi hiyo.
Nyota huyo anaondoka akiwa ameichezea Brazil michezo130, akifunga mabao 80 na kutoa pasi za mabao 59, rekodi hiyo inamfanya kubaki kinara wa mabao katika historia ya timu ya taifa ya Brazil.
Licha ya kutotwaa Kombe la Dunia akiwa na Brazil, Neymar alishiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na kuwa sehemu ya kikosi cha taifa kwa zaidi ya muongo mmoja.
Kwa takwimu na mchango wake ndani ya timu ya taifa, Neymar anaondoka akiwa ameweka rekodi zinazobaki sehemu ya historia ya soka la Brazil.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment