Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno Christiano Ronaldo amehitimisha safari yake kwenye michuano ya kombe la Dunia ambayo rasmi ilianza mwaka 2006 na kutamatika mwaka 2026.
“Ninafurahia Kombe hili la Dunia, mashabiki na watu waliolizunguka. Na kwa hakika hili litakuwa Kombe langu la Dunia la mwisho, uamuzi tayari umefanyika.” alisema Ronaldo.
Mwisho wa zama za Ronaldo umehitimishwa mara baada ya Ureno kuondolewa hatua ya 16 bora kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Hispania, matokeo hayo yamekatisha ndoto za staa huyo kunyanyua kombe la Dunia Licha ya kucheza makala sita za mashindano hayo
Mafanikio makubwa aliyo yapata staa huyo ndani ya mashindano hayo ni kufika hatua ya nusu fainali mwaka 2006, huku mwaka 2010 akifikia hatua ya 16 bora, 2014 hatua ya makundi, 2018 hatua ya 16 bora, 2022 robo fainali, 2026 hatua ya 16 bora.
Licha ya kabati lake kukosa ubingwa wa kombe la Dunia, Ronaldo atabaki kwenye vichwa vya wapenzi wa soka Duniani kutokana na makubwa aliyowahi kuyafanya akiwa kwenye ngazi ya vilabu mpaka timu ya Taifa, hakika mpira wa miguu hautalisahu jina la staa huyo.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment