MNYAMA AUNGURUMA BAADA YA MISIMU MINNE

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Simba SC imetwaa ubingwa wa Kombe la CRDB Federation Cup 2025/26 baada ya kuifunga Azam FC bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa Uwanja wa Gombani, Pemba.

Ushindi huo umehitimisha ukame wa misimu minne kwa Simba bila kutwaa taji hilo, ambapo mara ya mwisho ililibeba msimu wa 2020/21 ,bao pekee la mchezo lilifungwa dakika ya 62 baada ya kiungo wa Azam FC, Yahya Zayd, kujifunga alipokuwa akijaribu kuondoa hatari langoni kwake.

Matokeo hayo yameifanya Simba kutwaa Kombe la FA kwa mara ya nne tangu mashindano hayo yaliporejea msimu wa 2015/16, Kwa upande wa Azam FC, kipigo hicho kimehitimisha safari yao na ndoto yao ya kutwaa kikombe msimu huu.

Ubingwa huo umekata kiu ya klabu ya Simba ambapo kwa misimu minne mfululizo imeshindwa kunyanyua kombe la ligi kuu wala FA, lakini msimu huu 2025/26 wamefanikiwa kuondoa mkosi wa kutoshinda makombe baada ya kushinda vikombe viwili FA , na kombe la Muungano.

Mashindano hayo yamehitimisha msimu na sasa vilabu vinajipanga na msimu mpya wa mashindano 2026/27 ambapo Kuna takribani mwezi mmoja kuelekea msimu mpya wa mashindano.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments