MESSI AMTOLEA UVIVU MWAMUZI RAIA WA URENO

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Nahodha wa Argentina, Lionel Messi, alionekana akiingia kwenye majibizano mafupi na mwamuzi João Pinheiro raia wa Ureno wakati wa mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Uswisi, akimtaka amheshimu katika mawasiliano yao uwanjani.

Tukio hilo limetokea katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 kabla ya Argentina kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kutinga hatua ya nusu fainali kwenye mashindano hayo.

"Usinidharau tafadhali zungumza nami kwa heshima Mimi ninazungumza nawe kwa heshima, hivyo usinidharau" alisema Messi.

Hili ni miongoni mwa matukio machache kumuona Messi akiingia kwenye majibizano ya aina hiyo na mwamuzi, jambo lililovuta hisia kutokana na namna ambavyo mshambuliaji huyo amekuwa akijulikana kwa utulivu wake anapokuwa uwanjani.


Inaoneka mwamuzi aliongea kauli kwa lugha isiyokuwa ya kistaarabu dhidi ya nyota huyo bila kujali hadhi ya staa huyo, ndio maana pasipo kutarajiwa ilimlazimu staa huyo kutoa kauli hiyo kuhitaji heshima anayostahili.

Licha ya tukio hilo, Messi aliendelea kuiongoza Argentina hadi kupata ushindi dhidi ya Uswisi katika mchezo huo wa robo fainali, matokeo yaliyowahakikishia nafasi ya kucheza hatua ya nusu fainali kombe la Dunia.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments