Mbappe aweka historia upachikaji mabao kwenye mashindano makubwa matatu

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe ametikisa ulimwengu wa soka kwa rekodi ya aina yake kwenye upachikaji wa mabao akifanya hivyo kwenye mashindano makubwa aliyo shiriki na hatimaye kukwea kilelele Cha ufungaji Duniani.

Baada ya kufunga bao mbili kwenye mchezo wa mshindi wa tatu dhidi ya England, Mbappe anafikisha mabao 10 na kuongoza orodha ya wafungaji bora kombe la Dunia 2026 nyuma ya Lionel Messi mwenye mabao 8, pia amefikisha mabao 22 na kuwa ndie mfungaji bora wa Muda wote kombe la Dunia nyuma ya Messi mwenye mabao 21, chakuvutia zaidi ndie mfungaji bora wa UEFA na Laliga mwaka huu.

Historia hiyo itasimama iwapo mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi asipofunga bao kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Spain, iwapo Messi atafunga bao Moja mizani katika ufungaji Bora wa Dunia kwa muda wote itakuwa sawa na iwapo Messi atafunga bao mbili atakuwa mfungaji bora wa muda wote kombe la Dunia na kuharibu historia iliyotangulizwa na Kylian Mbappe.

Msimu wa Mbappe umekuwa kama ifuatavyo.

Mfungaji bora laliga: 25

Mfungaji bora UEFA: 15

Mfungaji bora muda wote WC: 22

Mfungaji bora mpaka sasa WC: 10.

Mchezo wa fainali kati ya Argentina na Spain ndio utakao amua hatima ya Mbappe kwenye historia ya upachikaji mabao kombe la Dunia, na hatima hiyo ipo mikononi mwa Lionel Messi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments