Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mataifa sita yamejihakikishia kushiriki Kombe la Dunia la FIFA 2030 baada ya kuthibitishwa kuwa waandaaji wa mashindano hayo.
Hispania, Ureno na Morocco zitakuwa wenyeji wakuu wa mashindano, huku Uruguay, Argentina na Paraguay zikipokea baadhi ya mechi maalumu za maadhimisho ya miaka 100 tangu kufanyika kwa Kombe la Dunia la kwanza mwaka 1930.
Kwa mujibu wa kanuni za FIFA, kila taifa linaloandaa mashindano hupata tiketi ya moja kwa moja ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia.
Uruguay itakuwa mwenyeji wa mechi ya ufunguzi ikiwa sehemu ya kumbukumbu ya historia ya mashindano hayo, yaliyoanza nchini humo mwaka 1930. Argentina na Paraguay pia zitakuwa sehemu ya waandaaji, ambapo Argentina imehusishwa na maadhimisho ya karne moja ya Kombe la Dunia, huku Paraguay ikichaguliwa kutokana na kuwa makao makuu ya Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (CONMEBOL).
Kutokana na uamuzi huo, Hispania, Ureno, Morocco, Uruguay, Argentina na Paraguay zimefuzu moja kwa moja kushiriki Kombe la Dunia la FIFA 2030.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.

Post a Comment