MAREKANI MABEGANI MWA FIFA, NAFUU YAPATIKANA KUELEKEA KUWAVAA UBELGIJI

 

Timothy Lugembe ,

Mwanakwetusports.

Mshambuliaji wa Marekani Folarin Balogun atakuwa sehemu ya kikosi cha Marekani katika mchezo wa hatua ya 16 Bora dhidi ya Ubelgiji, licha ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa hatua ya 32 Bora dhidi ya Bosnia na Herzegovina.

Balogun alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 64 katika mchezo huo baada ya tukio lililomuhusisha mlinzi wa Bosnia, Tarik Muharemovic, Kwa kawaida, kadi nyekundu ya moja kwa moja humfanya mchezaji akose mchezo unaofuata ndiyo maana baada ya tukio hilo ilitarajiwa wazi kwamba angeikosa Marekani dhidi ya Ubelgiji.

Hata hivyo, mambo yamebadilika baada ya FIFA kuingilia uamuzi huo, Kamati ya Nidhamu ya FIFA imesema adhabu ya kusimamishwa mchezo mmoja bado ipo, lakini utekelezaji wake umeahirishwa kwa kipindi cha mwaka mmoja wa majaribio. Kwa maana hiyo, Balogun hatatumikia adhabu hiyo sasa, na badala yake ataruhusiwa kucheza dhidi ya Ubelgijinhuku adhabu hiyo itarudi kutekelezwa endapo atafanya kosa jingine la aina inayofanana ndani ya kipindi hicho. 

Hapo ndipo mjadala ulipoanzia, Swali limekuwa hili, kama alionyeshwa kadi nyekundu na sheria zinasema mchezaji wa aina hiyo anakosa mchezo unaofuata, kwa nini Balogun amepewa nafasi ya kucheza? Jibu lake liko kwenye namna FIFA ilivyotumia mamlaka yake ya kinidhamu, wakati kanuni za mashindano ya Kombe la Dunia zinaeleza kuwa mchezaji anayetolewa kwa kadi nyekundu anasimamishwa moja kwa moja mchezo unaofuata, FIFA imetumia kipengele cha nidhamu kinachoruhusu kusimamisha utekelezaji wa adhabu kwa muda. Hivyo, kadi haijafutwa, lakini adhabu yake imewekwa pembeni kwa sasa. 

Kwa upande wa Marekani, habari hii inabadilisha maandalizi ya mchezo dhidi ya Ubelgiji. Balogun alikuwa tayari ameonyesha mchango wake katika michuano hii akiwa amepachika mabao matatu, hivyo kurejea kwake kunamaanisha Marekani inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na mshambuliaji wake badala ya kutafuta mbadala wake Lakini pamoja na kurejea kwake, Balogun sasa atakuwa chini ya tahadhari ya nidhamu, kwa sababu kosa jingine ndani ya muda huo wa majaribio linaweza kufanya adhabu ile ile irudi na kutekelezwa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments