Kuondolewa Kombe la Dunia Kwamng’oa Pape Thiaw Senegal

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Senegal, Pape Thiaw, amejiuzulu rasmi nafasi yake siku chache baada ya Senegal kuondolewa kwenye hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia 2026 kufuatia kufungwa mabao 3-2 dhidi ya Ubelgiji.

Kujiuzulu kwa Thiaw kunakuja wakati ambao tayari kulikuwa na mvutano ndani ya kambi ya Senegal, hasa baada ya kiungo Pape Gueye kutangaza kuwa atasitisha kuichezea timu ya taifa iwapo benchi la ufundi lingeendelea kubaki chini ya kocha huyo.

Gueye alitoa msimamo huo baada ya mchezo wa Senegal dhidi ya Ubelgiji, ambapo alitolewa dakika ya 66 wakati wakiwa mbele kwa bao 2-0 tukio ambalo lilionekana kutomfurahisha, Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao ya kijamii , kiungo huyo wa Villarreal alisema kwa sasa hatakuwa tayari kuendelea kuitumikia Senegal ikiwa benchi hilo la ufundi lingeendelea kuwepo, huku akiahidi kuzungumzia kwa kina sababu za uamuzi wake baadaye.

Kauli ya Gueye ilikuja mara baada ya Senegal kushindwa kuendeleza matumaini yao ya kusonga mbele katika mashindano hayo ilihali walikuwa na nafasi kubwa ya kufikia hatua za mbali katika mashindano hayo, jambo lililoongeza mjadala kuhusu mwenendo wa timu hiyo na maamuzi ya benchi la ufundi.

Katika hatua iliyofuata, shinikizo hilo limezaa mabadiliko baada ya Thiaw kutangaza kuachia ngazi kama kocha mkuu wa Senegal, Uamuzi huo unafungua ukurasa mpya ndani ya timu ya taifa ya Senegal, ambayo sasa inatarajiwa kuanza mchakato wa kufanya mabadiliko ya kiufundi kuelekea mashindano yajayo.

Kuondoka kwa Thiaw kunaonekana kuhusiana moja kwa moja na kauli ya Gueye, ambaye aliweka wazi kuwa mustakabali wake na timu ya taifa ungeamuliwa na hatma ya benchi la ufundi, mashabiki na Wadau wasoka wanaamini kocha alishindwa kuchanga karata zake vyema na kujikita anafanyia mabadiliko yaliyo igharim timu.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com





0/Post a Comment/Comments