Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Waandaaji wa tuzo ya Ballon d'Or wametoa ufafanuzi kuhusu
mjadala unaoendelea wa vigezo vya kumpata mshindi, wakieleza kuwa kutwaa Kombe
la Dunia pekee hakutoshi kumhakikishia mchezaji kushinda tuzo hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo hayo, mafanikio katika mashindano ya
kimataifa ni sehemu ya tathmini, lakini uamuzi wa mwisho huzingatia kiwango cha
mchezaji katika msimu mzima, mchango wake kwa klabu na timu ya taifa pamoja na
takwimu binafsi.
Kauli hiyo imeendelea kuzua mjadala kuhusu nani anaweza kuwa
mbele katika kinyang'anyiro cha Ballon d'Or. Wengi wanamtaja Kylian Mbappe kuwa
na nafasi kubwa kutokana na mafanikio yake binafsi katika msimu uliopita.
Mbappe alimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa La Liga, UEFA Champions League na Kombe la Dunia aidha, ameendelea kuweka rekodi kwa kuwa mfungaji bora wa muda wote katika mashindano ya kombe la Dunia.
Kutokana na takwimu hizo na vigezo vilivyowekwa na waandaaji
wa Ballon d'Or, mjadala umehamia kwenye mchango wa mchezaji kwa msimu mzima
badala ya kutegemea ubingwa wa Kombe la Dunia pekee huku Mbappe akiwa mbele kwa
takwimu binafsi licha ya kutokuwa na ubingwa.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment