FIFA yaweka wazi muda wa mapumziko fainali ya Kombe la Dunia

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Baada ya mjadala wa muda mrefu kuhusu muda wa mapumziko ya kipindi cha kwanza katika fainali ya Kombe la Dunia 2026, Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeweka wazi kuwa mapumziko hayo hayatakuwa dakika 30 kama ilivyokuwa ikidaiwa, bali yatabaki kuwa dakika 17.

Taarifa hiyo inafuatia taarifa zilizosambaa kwa wiki kadhaa zikidai kuwa fainali hiyo itakuwa na burudani ya muziki wakati wa mapumziko, jambo ambalo lingesababisha kipindi cha mapumziko kuongezwa hadi dakika 30.

Pendekezo hilo lilizua mjadala mkubwa ndani ya dunia ya soka, huku baadhi ya wachezaji wa zamani na wadau wa mchezo wakieleza kuwa kuongeza muda wa mapumziko kungeweza kuathiri utayari wa wachezaji kuelekea kipindi cha pili. Hoja yao ilikuwa kwamba mchezo kusimama kwa muda mrefu kungepunguza kasi ya mchezo na kuathiri hali ya mwili kwa wachezaji.

Hata hivyo, FIFA imefafanua kuwa muda wa mapumziko hautabadilika, Kwa mujibu wa mpangilio uliotolewa, dakika 11 zitatumika kwa burudani ya muziki, huku dakika sita zikielekezwa kwenye maandalizi na kuondoa jukwaa pamoja na shughuli za matengenezo ya uwanja, ikiwemo umwagiliaji.

Kwa uamuzi huo, muda wa mapumziko katika fainali ya Kombe la Dunia 2026 utabaki kuwa dakika 17, huku FIFA ikiondoa sintofahamu iliyokuwa imejitokeza kuhusu uwezekano wa kuongeza muda huo hadi dakika 30.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments