Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeanza kujadili pendekezo la kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki Kombe la Dunia la mwaka 2030 kutoka 48 hadi 64.
Rais wa FIFA, Gianni Infantino, amesema pendekezo hilo linalenga kutoa nafasi kwa mataifa mengi zaidi kushiriki mashindano hayo huku likiendelea kukuza maendeleo ya soka duniani na kuhakikisha mataifa mengi ambayo haijawahi kushiriki kombe hilo kukamilisha ndoto wanazo ziota kwa miaka mingi.
kama pendekezo hilo litapitishwa, timu 16 zitaongezwa kutoka mfumo wa sasa wa timu 48, ambao utaanza kutumika katika Kombe la Dunia la mwaka 2030, ikumbukwe kuwe kombe la Duniana la mwaka huu limepata nyongeza ya timu 16 nakufikia idadi ya timu 48 kutoka 32 kwenye mashindano yaliyopita.
Kombe la Dunia la mwaka 2030 litafanyika katika mataifa sita ambapo Uruguay, Argentina na Paraguay zitaandaa michezo ya ufunguzi, huku michezo iliyosalia ikifanyika Morocco, Hispania na Ureno.
Pendekezo hilo limeibua mjadala miongoni mwa wadau wa soka duniani, Wapo wanaoamini kuwa ongezeko hilo litatoa nafasi kwa mataifa mengi zaidi kushiriki mashindano hayo, wakati wengine wakieleza kuwa linaweza kuathiri ushindani wa michuano hiyo na kufanya mashindano yakakosa radha kutokana na wingi wa timu shiriki.
0767815473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment