FIFA yafungua uchunguzi baada ya vurugu kwenye fainali ya Kombe la Dunia

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeanzisha uchunguzi kuhusu tukio la vurugu lililotokea mara baada ya mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia uliomalizika kwa Hispania kuifunga Argentina bao 1-0 na kutwaa ubingwa.

Mchezo ulipomalizika, hali ya sintofahamu ilizuka uwanjani huku baadhi ya wachezaji wa timu hizo wakihusika katika mabishano yaliyogeuka ugomvi mbele ya waamuzi na maofisa wa mchezo.

Taarifa zinaeleza kuwa beki wa Argentina, Nahuel Molina, alionekana kumpiga kiungo wa Hispania Rodri kabla ya ugomvi huo kuendelea na kuwahusisha Gavi, Leandro Paredes pamoja na Eric García.

Kutokana na tukio hilo, FIFA imesema itakusanya ushahidi na kupitia taarifa za waamuzi pamoja na picha za video ili kubaini kilichotokea kabla ya kufikia uamuzi dhidi ya wachezaji watakaobainika kukiuka kanuni za mchezo.

"FIFA itachunguza kwa kina kilichotokea kabla ya kuamua hatua zinazofaa kuchukuliwa dhidi ya wachezaji waliohusika," imeeleza taarifa ya FIFA.

Hatua hiyo inatarajiwa kubaini iwapo wachezaji waliotajwa watakabiliwa na adhabu za kinidhamu kulingana na kanuni za FIFA, huku shirikisho hilo likisisitiza umuhimu wa kulinda nidhamu na heshima ya mchezo baada ya kumalizika kwa mashindano.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments