EA Sports yafanikiwa kutabiri mshindi wa kombe la Dunia kwa mara ya tano mfululizo

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kampuni ya michezo ya video ya EA Sports imeendelea kuthibitisha rekodi yake ya kutabiri mabingwa wa Kombe la Dunia baada ya Spain kutwaa taji la mwaka 2026 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina katika mchezo wa fainali uliofanyika nchini Marekani.

Matokeo hayo yameufanya utabiri wa kampuni hiyo, uliotolewa kabla ya kuanza kwa mashindano kupitia mfumo wa simulation, kuwa sahihi kwa mara nyingine baada ya kuonesha kuwa Spain ingeibuka bingwa wa dunia.

Kabla ya kuanza kwa michuano, utabiri wa EA Sports ulizua mjadala miongoni mwa mashabiki na wachambuzi wa soka, wapo walioamini rekodi ya kampuni hiyo kutokana na kufanikiwa kutabiri mabingwa wa Kombe la Dunia wa mwaka 2010, 2014, 2018 na 2022, huku wengine wakieleza kuwa matokeo ya mashindano huamuliwa uwanjani.

Katika utabiri huo, Spain ilipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa kutokana na tathmini ya mfumo wa simulation uliotumia takwimu za ubora wa kikosi, uwezo wa wachezaji, mfumo wa uchezaji na matokeo ya siku za karibuni.

Ushindi huo umeifanya EA Sports kuendelea kuwa na rekodi ya kutabiri kwa usahihi mabingwa wa Kombe la Dunia, baada ya utabiri wake kuhusu Spain kuendana na matokeo ya mashindano yaliyofanyika Marekani, Canada na Mexico.

Hili linakuwa kombe la Dunia la pili kwa Spain kutwaa huku wakiwa hawajafungwa kwenye mchezo wa fainali kwenye michuano hiyo.

WASHINDI WA TUZO KOMBE LA DUNIA

Rodri - mchezaji bora wa mashindano 

Kylian Mbappe - Mfungaji Bora wa mashindano 

Unai Simon - kipa Bora wa mashindano

Pau Curbas - mchezaji bora chipukizi wa mashindano.


0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.




0/Post a Comment/Comments