Colombia wataka kutoka na roho ya mtu kisa Kombe la Dunia

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Shirikisho la Soka la Colombia (FCF) limezitaka mamlaka za usalama kuchunguza vitisho vya kuuawa vinavyomkabili mshambuliaji Jamilton Campaz baada ya mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Switzerland.

Campaz ameingia kwenye taharuki baada ya kupokea ujumbe wa vitisho kutoka kwa baadhi ya mashabiki wenye hasira kufuatia kukosa nafasi ya kufunga katika dakika za nyongeza, jambo lililochangia Colombia kuondolewa kwenye mashindano hayo kufuatia kufungwa kwa mikwaju ya penati 4-3.

Kutokana na hali hiyo, mchezaji huyo ameripotiwa kujificha na kukataa kurejea nchini kwa hofu ya usalama wake huku vitisho dhidi yake vikiendelea kusambazwa.


FCF imelaani tukio hilo na kusisitiza kuwa tofauti za kimichezo hazipaswi kugeuka sababu ya kuhatarisha maisha ya mtu.

Shirikisho hilo limeongeza kuwa linaendelea kushirikiana na mamlaka za usalama kuhakikisha Campaz anapatiwa ulinzi unaohitajika huku uchunguzi ukiendelea kuwabaini waliotuma vitisho hivyo.

Tukio hilo limezua mjadala kuhusu ongezeko la vitendo vya chuki dhidi ya wachezaji baada ya matokeo ya michezo, huku wadau wengi wakikumbusha kuwa ushindi na kushindwa ni sehemu ya soka, lakini maisha ya binadamu yanapaswa kulindwa wakati wote.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com



0/Post a Comment/Comments