Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Klabu ya Chelsea imeanza mchaka wa kumsajili mshambuliaji Danny Welbeck kutoka Brighton & Hove Albion kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Welbeck, mwenye umri wa miaka 35, amebakiza miezi 12 katika mkataba wake na Brighton, huku klabu hiyo ikifahamu kuwapo kwa nia ya Chelsea ya kumhitaji.
Taarifa zinaeleza kuwa kocha wa Chelsea, Xabi Alonso, anamuona Welbeck kuwa mchezaji anayefaa katika kikosi chake kutokana na uzoefu wake ndani ya uwanja na nafasi yake ya uongozi kwenye timu.
Hata hivyo, mazungumzo hayo bado yako katika hatua za awali na hakuna makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo.
Iwapo mazungumzo yataendelea kwa mafanikio, Welbeck anaweza kuondoka Brighton na kujiunga na Chelsea kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment