Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Beki wakati wa Simba SC, Chamou Karaboue, ameaga rasmi klabu hiyo baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miwili klabuni hapo , akiwashukuru viongozi, benchi la ufundi, wachezaji wenzake na mashabiki wa klabu hiyo kwa kipindi alichokitumikia.
Karaboue, ambaye alitolewa kwa mkopo kujiunga na TRA United katika nusu ya pili ya msimu uliomalizika, alitoa ujumbe huo kupitia kurasa yake kwenye mtandao wa kijamii akieleza kuwa kila safari ina mwanzo na mwisho, na sasa umefika wakati wa kusema kwaheri kwa familia ya Simba.
Katika ujumbe wake, beki huyo kutoka Ivory coast amesema anaondoka akiwa na shukrani kwa kila wakati alioupitia ndani ya klabu, masomo aliyojifunza na watu aliokutana nao, akisisitiza kuwa ataendelea kubeba kumbukumbu za Simba moyoni mwake.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment