Bayern yatoa msimamo wake kuhusu Olise na Luis Diaz


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Bayern Munich imeondoa uwezekano wa kuwauza Michael Olise na Luis Díaz baada ya Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Uli Hoeneb kuweka wazi kuwa hakuna mazungumzo yoyote yanayohusu kuondoka kwa wachezaji hao katika dirisha la usajili.

Kauli hiyo imekuja kufuatia taarifa zilizokuwa zikihusisha Real Madrid na Olise, huku Rais huyo akisema taarifa hizo hazina msingi kwa kuwa kiungo huyo bado ana miaka mitatu ya mkataba wake na Bayern.

Aidha, Hoeneß alisema msimamo huo hauishii kwa Olise pekee, bali unamhusu pia Luis Díaz, akieleza kuwa klabu haitakuwa tayari kujadili uhamisho wa mchezaji yeyote kati yao hata kama kutatokea ofa kutoka klabu nyingine.

Ameongeza kuwa , Bayern imejenga safu yake ya ushambuliaji ikiwajumuisha Olise, Díaz na Harry Kane, hivyo klabu inaendelea na mipango yake ikiwa na wachezaji hao na haina mpango wa kuwauza katika kipindi hiki cha usajili.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.





0/Post a Comment/Comments