BARCOLA MAMBO SAFI KUTUA ANFIELD

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Liverpool imeendelea na juhudi za kumsajili winga Bradley Barcola kutoka Paris Saint-Germain (PSG), huku mchezaji huyo akitajwa kuwa chaguo la kwanza la klabu hiyo katika kuimarisha safu ya ushambuliaji.

Taarifa zinaeleza kuwa Liverpool imekuwa ikimfuatilia Barcola tangu dirisha la usajili la mwaka 2025 na imeendelea kufanya kazi ya kufanikisha uhamisho huo tangu Aprili mwaka huu, Mazungumzo yanategemea makubaliano ya ada ya uhamisho ambayo PSG itaweka.

Barcola ameripotiwa kuwa yuko tayari kujiunga na Liverpool iwapo klabu hizo mbili zitafikia makubaliano, huku akitoa kipaumbele kwa mradi wa Liverpool kuliko ofa nyingine zinazoweza kujitokeza.

Wakati huohuo, mchezaji huyo amefanya uamuzi wa kutosaini mkataba mpya na PSG ambapo Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika Juni 2028, lakini taarifa zinaeleza kuwa hataongeza mkataba, jambo linalofungua uwezekano wa kuondoka katika dirisha hili la usajili.

Kutokana na hali hiyo, Liverpool inaendelea kusubiri PSG itangaze kiwango cha mwisho cha ada ya uhamisho kabla ya kuendelea na hatua zinazofuata za mazungumzo.

Iwapo makubaliano yatafikiwa, Barcola ataondoka PSG baada ya kuamua kutafuta changamoto mpya, huku Liverpool ikionekana kuwa mbele katika mbio za kupata saini yake.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments