Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mshambuliaji wa Portugal Cristiano Ronaldo ameendelea kuiweka hai ndoto katika Kombe la Dunia baada ya kufunga bao lililoisaidia timu hiyo kuiondoa Croatia na kusonga mbele hadi hatua ya 16 Bora kufuatia ushindi wa 2-1 katika dakika tisini.
Ronaldo aliifungia Portugal bao dakika ya 68 kwa mkwaju wa penalti, katika mchezo wa hatua ya mtoano, Kwa bao hilo, nahodha huyo wa Portugal ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia, akifanya hivyo akiwa na miaka 41 na kufikisha mabao matatu katika mashindano hayo.
Ushindi huo umeifanya Portugal kusalia kwenye mbio za kusaka taji la dunia, huku macho sasa yakielekezwa kwenye mchezo ujao wa hatua ya 16 Bora dhidi ya Spain Mchezo ambao unatarajiwa kupigwa Julai 6, 2026, ukiwa ni njia ya kutinga robo fainali.
Kwa Ronaldo, hatua hiyo inafungua ukurasa mwingine katika safari yake ya mwisho ya Kombe la Dunia, Licha ya kuwa na mafanikio makubwa katika soka la klabu na timu ya taifa, bado hajawahi kulitwaa taji la Kombe la Dunia, jambo linaloifanya safari hii kuwa muhimu kwake binafsi na kwa taifa la Portugal.
Sasa mtihani unaofuata uko mbele ya Spain, timu ambayo nayo inaingia hatua hiyo ikiwa na lengo la kutinga robo fainali , Kwa Ronaldo na wenzake, huo utakuwa mchezo mwingine wa kuthibitisha kama ndoto ya kutwaa Kombe la Dunia bado ina nafasi ya kuendelea.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment