Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Baada ya kushindwa kukutana katika mchezo wa Finalissima, sasa Spain na Argentina zitachuana katika fainali ya Kombe la Dunia 2026, zikiwa na nafasi ya kuamua bingwa wa dunia huku Kila timu ikiwa ni bingwa wa bara lake.
Awali, timu hizo zilitarajiwa kukutana katika Finalissima baada ya Spain kutwaa ubingwa wa Euro 2024 na Argentina kushinda Copa America 2024. Mechi hiyo ilikuwa imepangwa kufanyika Machi 27, 2026, nchini Qatar, lakini haikufanyika kutokana na sababu zilizohusisha ratiba ya mashindano ya kimataifa na baadaye changamoto za kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati, hali iliyofanya UEFA na CONMEBOL kushindwa kupata tarehe na maandalizi mbadala yaliyofaa.
Kutokana na Kuhaurishwa kwa mchezo huo kuliondoa nafasi ya mabingwa hao wa mabara mawili kupimana nguvu, huku wadau wa soka wakisubiri kwa muda mrefu kuona timu hizo zikikutana na sasa rasmi miamba hiyo itakutana Julai 19, 2026.
Argentina inaingia kwenye fainali hiyo ikiwa inawania ubingwa wake wa nne wa Kombe la Dunia, baada ya kutwaa mataji matatu yaliyopatikana mwaka 1978, 1986 na 2022. Kwa upande wa Spain, inatafuta taji la pili baada ya kushinda ubingwa wake wa kwanza mwaka 2010.
Hivyo, mchezo ulioshindikana kuchezwa kupitia Finalissima sasa umehamia kwenye jukwaa la Kombe la Dunia, ambapo bingwa mpya wa dunia ataamuliwa kati ya mabingwa wa Ulaya na mabingwa wa Amerika Kusini.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment