Ayoub Bouaddi anukia City baada ya kufanya vizuri Kombe la Dunia

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Manchester City imeendelea na mazungumzo ya kumsajili kiungo chipukizi Ayoub Bouaddi kutoka Lille, kufuatia kiwango alichoonyesha akiwa na timu ya taifa ya Morocco katika michuano ya Kombe la Dunia.

Taarifa zinaeleza kuwa mazungumzo yanaendelea kati ya Manchester City, Lille na wawakilishi wa mchezaji huku pande zote zikijadili masharti ya kufanikisha uhamisho huo, Klabu hiyo ya Ligi Kuu England inakabiliwa na ushindani kutoka kwa timu nyingine zinazomfuatilia Bouaddi.

City inatafakari iwapo itakamilisha usajili huo katika dirisha la sasa la usajili au kusubiri hadi mwaka 2027, hatua itakayozingatia makubaliano yatakayofikiwa na pande zote.

Bouaddi ameendelea kuvutia baada ya mchango wake akiwa na Morocco, jambo lililoongeza idadi ya klabu zinazotaka huduma yake, Endapo mazungumzo yatakamilika, kiungo huyo anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Manchester City katika msimu ujao au kujiunga baadaye kulingana na makubaliano yatakayofikiwa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments