ARSENAL YAMNYATIA VINICIUS JR

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Klabu ya Arsenal imeanza kufuatilia kwa karibu saini ya mshambuliaji wa Real Madrid Vinicius Jr wakati ambao mazungumzo ya kuongeza mkataba na klabu yake yakiwa bado hayajafikia muafaka.

Taarifa zinaeleza kuwa klabu hiyo ya Ligi Kuu England imeonyesha nia ya awali ya kumleta mshambuliaji huyo wa Brazil endapo mazungumzo yake na Real Madrid yatashindikana.

Vinicius bado ana mkataba na Real Madrid, lakini hadi sasa hajatia saini mkataba mpya licha ya mazungumzo kati ya pande hizo kuendelea.

Kwa sasa, mazunguzo yanaendelea ya kumbakisha nyota huyo, huku Arsenal ikisubiri kuona mwelekeo wa mazungumzo kabla ya kuamua hatua zinazofuata kwenye dirisha la usajili.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments