Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Timu ya taifa ya Argentina imefuzu hatua ya robo fainali michuano ya kombe la Dunia 2026, kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Misri katika mchezo wa hatua ya 16 Bora uliopigwa katika dimba la Atlanta nchini Marekani.
Katika mchezo huo, Misri walionyesha ukomavu kiuchezaji baada ya kuingoza kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 79, lakini hadithi hiyo iligeuka simanzi kwa mafarao baada ya ubao kugeuka kwa dakika 17 za mwisho na Argentina kutoka nyuma na kushinda 3-2 na kujikatia tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali.
Matokeo hayo ni dhahiri kuwa ugonjwa wa timu kutoka Afrika ni ule ule, baada ya Misri kushindwa kulinda matokeo waliyokuwa nayo na kuondoshwa kwenye michuano hiyo. Ikumbukwe kuwa awali timu za Senegal, Afrika kusini, Ivory coast na Congo DR zilishindwa kusonga mbele hatua inayofuata kutokana na kushindwa kulinda matokeo waliyokuwa nayo katika dakika za mwisho.
Mpaka sasa, Afrika imebakiza muwakilishi mmoja katika michuano hiyo ambaye ni Morocco na atacheza robo fainali dhidi ya timu ya taifa ya ufaransa siku ya Julai 9, 2026.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment