Wenyeji wa Kombe la Dunia 2026 Watinga Hatua ya 32 Bora

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mataifa mwenyeji wa Kombe la Dunia 2026, Marekani, Mexico na Canada, yameendelea kufanya vizuri katika hatua ya makundi huku Marekani na Mexico zikijihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya 32 bora, wakati Canada ikisalia na hatua moja kuelekea kufuzu.

Marekani imefuzu baada ya kushinda michezo yake miwili ya kundi D , Katika mchezo wa kwanza iliifunga Paraguay mabao 4-1 kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Australia, matokeo yaliyoifanya kufikisha alama sita kileleni mwa kundi hilo.

Mexico nayo imefuzu baada ya kuanza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Afrika Kusini na baadaye kuifunga Korea Kusini bao 1-0, Ushindi huo umeifanya kufikisha alama sita na kuongoza kundi A.

Kwa upande wa Canada, imekusanya alama nne katika michezo miwili ya kwanza kundi B, timu hiyo ilianza kwa sare ya mabao 1-1 dhidi ya Bosnia na Herzegovina kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Qatar katika mchezo wake wa pili.

Matokeo hayo yanaifanya Canada kuhitaji angalau sare katika mchezo wake wa mwisho wa kundi ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya 32 bora.

Kwa matokeo hayo, mataifa mwenyeji yameonyesha mwanzo mzuri katika mashindano hayo, huku yakisubiri kukamilika kwa hatua ya makundi kabla ya kuanza kwa michezo ya mtoano, hata hivyo timu hizo zinatarajia kuingia katika mzunguko wa tatu hatua ya makundi ili kukamilisha rataiba huku Canada wakihitaji alama yoyote ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu 

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments