Uholanzi yaendeleza rekodi ya kutofungwa kwa miaka 20, Morocco ikitinga hatua ya 16 bora

 


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya Taifa ya Morocco imefuzu hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kuiondoa Uholanzi kwa ushindi wa penalti 3-2, kufuatia sare ya 1-1 iliyodumu kwa dakika 120 katika mchezo wa hatua ya 32 bora.

Matokeo hayo yanaifanya Uholanzi kuendelea kushikilia rekodi ya kutopoteza mchezo wowote wa Kombe la Dunia ndani ya dakika 90 tangu mwaka 2006, ikiwa sasa imetimiza miaka 20 bila kufungwa katika muda wa kawaida wa mchezo.

Hata hivyo, rekodi hiyo haikutosha kuipeleka mbele kwenye mashindano hayo, kwani iliondolewa kwa mikwaju ya penalti kwa mara nyingine katika hatua ya mtoano ikumbukwe kuwa Mwaka 2010 ilipoteza fainali dhidi ya Hispania baada ya kufungwa katika dakika 120 za nyongeza, mwaka 2014 iliondolewa na Argentina kwa mikwaju ya penalti, mwaka 2018 haikufuzu Kombe la Dunia, mwaka 2022 iliondolewa kwa penalti na Argentina, na sasa mwaka 2026 imeondolewa na Morocco kwa penalti.

Kwa upande wa Morocco, ushindi huo unaifanya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu hatua ya 16 bora katika Kombe la Dunia 2026, huku Afrika Kusini ikiwa tayari imeaga mashindano hayo na kupunguzwa idadi ya timu kutoka Afrika wakati ambao michezo inaendelea.

Morocco, ambayo ipo nafasi ya saba kwenye viwango vya FIFA, iliiondoa Uholanzi iliyo nafasi ya nane, na sasa itakutana na Canada katika hatua ya 16 bora Julai 4, 2026, kuwania tiketi ya robo fainali.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com





0/Post a Comment/Comments