TIMU YA TAIFA YA UFARANSA YAKUMBWA NA MAJONZI

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amekumbwa na msiba kufuatia kufiwa na mama yake, hali iliyomlazimu kuondoka kambini na kurejea nyumbani kwa ajili ya kuwa pamoja na familia yake katika kipindi hicho kigumu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyothibitishwa na Shirikisho la Soka la Ufaransa, Deschamps atasafiri kurejea nchini Ufaransa ili kushiriki shughuli za mazishi na kutoa heshima za mwisho kwa mama yake.

Kutokana na hali hiyo, Deschamps hatakuwepo benchi kuiongoza Ufaransa katika mchezo wao ujao dhidi ya Norway huku akitarajiwa kurejea wakati wa hatua ya mtoano ambapo timu yake tayali imefuzu.

Taarifa hiyo imeibua salamu za pole kutoka kwa wadau wa soka duniani, huku mashabiki na viongozi mbalimbali wakimtakia faraja yeye pamoja na familia yake katika kipindi hiki cha majonzi.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments