TIMU YA AFRIKA YA KWANZA KUONDOSHWA KOMBE LA DUNIA

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Timu ya Taifa ya Tunisia imeondolewa kwenye michuano ya Kombe la Dunia baada ya kupoteza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi kwa kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Japan.

Matokeo hayo yanakuja baada ya Tunisia kupokea kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya Sweden katika mchezo wa kwanza, hali iliyowaacha bila alama baada ya michezo miwili na kupoteza nafasi ya kufuzu hatua inayofuata ya mashindano.

Kwa kuondolewa huko, Tunisia inakuwa timu ya pili kufungasha virago katika michuano hiyo baada ya Uturuki, ambayo nayo ilishindwa kuendelea kwenye mashindano hayo kufuatia matokeo ya michezo yake ya hatua ya makundi.

Kwa upande wa bara la Afrika, Tunisia ndiyo timu ya kwanza kuondolewa rasmi kwenye mashindano hayo, hatua inayopunguza idadi ya wawakilishi wa Afrika wanaowania nafasi ya kutinga hatua ya mtoano.

Tunisia sasa itakamilisha ratiba yake hatua ya makundi kwa kucheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Uholanzi, ikiwa tayari imepoteza nafasi ya kusonga mbele, huku ikisaka kumaliza kampeni yake angalau wakiwa na alama.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments