Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Nyota wa timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameendelea kuandika historia katika soka la Dunia baada ya kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 5-0 wa Ureno dhidi ya Uzbekistan katika Kombe la Dunia 2026 na kupelekea kuandika historia mbili tofauti.
Kwa mabao hayo mawili, Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya soka kufunga mabao kwenye makala sita mfululizo ya Kombe la Dunia, akifunga katika michuano ya 2006, 2010, 2014, 2018, 2022 na sasa 2026.
Wengi wanaweza kujiuliza vipi kuhusu mashindani wake wa karibu ambaye ni Lionel Messi? Messi hakufanikiwa kufunga bao kwenye kombe la Dunia la mwaka 2010 lililo fanyika nchini Afrika kusini hivyo kumfanya Ronaldo kuwa ndio mchezaji pekee aliefunga katika mashindano hayo kwa mara sita mfululizo.
Pia nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 ameifikia rekodi ya mabao 10 katika historia ya Kombe la Dunia, na kuvunja rekodi ya ufungaji bora wa muda wote kwenye timu ya Taifa ya Ureno iliyokuwa ikishikiliwa na nguli Eusébio aliyekuwa na mabao tisa.
Mbali na hilo, Ronaldo ameendelea kuimarisha rekodi zake za kuwa mchezaji mwenye mechi nyingi zaidi na mabao mengi zaidi katika soka la kimataifa, huku akionyesha kuwa bado ni mmoja wa wachezaji muhimu wa Ureno katika michuano hiyo.
Mabao hayo mawili yalichangia Ureno kupata ushindi mkubwa wa kwanza kwenye Kombe la Dunia 2026 na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya mtoano wakiwa vinara wa kundi K na alama nne.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com


Post a Comment