PARTEY KUKOSA MCHEZO KOMBE LA DUNIA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kiungo wa Ghana Thomas Partey hataichezea timu yake katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Panama baada ya Mahakama ya Canada kutupilia mbali rufaa yake ya kupinga uamuzi wa kunyimwa visa ya kuingia nchini humo.

Partey alikuwa ameomba mahakama ibatilishe uamuzi wa mamlaka za uhamiaji za Canada zilizomzuia kuingia nchini humo siku chache kabla ya mchezo huo Hata hivyo, mahakama iliamua kuunga mkono uamuzi wa maafisa wa uhamiaji na hivyo kumzuia kushiriki michezo itakayochezwa Toronto.

Uamuzi huo unahusishwa na mashtaka yanayomkabili mchezaji huyo nchini Uingereza Partey anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono, huku akiendelea kukanusha tuhuma zote zinazomkabili.

Kutokana na hatua hiyo, Ghana italazimika kuanza kampeni yake ya Kombe la Dunia bila mmoja wa wachezaji wake wenye uzoefu mkubwa katika safu ya kiungo.

Wakati huo huo, taarifa zinaeleza kuwa Partey anatarajiwa kuruhusiwa kuingia Marekani, jambo ambalo linaweza kumwezesha kujiunga na kikosi cha Ghana katika michezo mingine ya hatua ya makundi itakayochezwa nchini humo.

Kwa upande wake, FIFA imeeleza kuwa masuala ya visa na uhamiaji yanabaki kuwa mamlaka ya nchi mwenyeji wa mashindano na si ya shirikisho hilo.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.




0/Post a Comment/Comments