ONANA KURUDI ALIKO TOKA

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Kipa wa Manchester United, Andre Onana, yuko hatua za mwisho za kurejea Trabzonspor ya Uturuki kwa mkopo baada ya klabu hizo kufikia makubaliano ya awali kuhusu uhamisho huo.

Makubaliano hayo yanatajwa kuwa ya mkopo yatakayodumu hadi Juni 2027, huku Trabzonspor ikikubali kulipa ada ya mkopo na pande zote zikiendelea kukamilisha taratibu za mwisho kabla ya kutangaza rasmi uhamisho huo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Onana kutokuwa sehemu ya mipango ya benchi la ufundi la Manchester United kuelekea msimu wa 2026/27, jambo lililoifanya klabu hiyo kuwa tayari kumruhusu kuondoka ili apate nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Onana aliitumikia Trabzonspor kwa mkopo msimu uliopita na kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza, hali iliyochangia klabu hiyo kuonyesha nia ya kumrejesha kwa kipindi kingine. Uamuzi wa Manchester United wa kumruhusu kuondoka unatajwa kuwa sehemu ya mipango ya kufanya mabadiliko kwenye kikosi kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Endapo hakutakuwa na mabadiliko ya dakika za mwisho, Onana atasafiri kuelekea Uturuki kwa ajili ya kukamilisha taratibu zilizobaki kabla ya kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa Trabzonspor kwa mkopo utakaomalizika Juni 2027.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments