✍️ EMMANUEL S. MASUZA
Mwanakwetu Sports
Dunia inatusahu ila Yale tuliwahi kuyafanya hayasahauliki sio kwamba yalikuwa bora sana ila pengine yalileta furaha sana kwa wanadamu wengine kiasi cha kuwafanya wasisahau Yale tuliyoyafanya hata kama dunia itatusaliti na kutusahu.
Nilikuwepo na kushuhudia ubora wa Ibrahim ajibu toka akiwa simba katika umri mdogo na badaye alipoenda yanga na kuonesha yeye ni nani nilishuhudia ubora uliotukuka wa kijana Huyu wa kiswahili daaah sijui niseme nini kuhusu ajibu maana ni zaidi ya mchezaji mzawa aliyebarikiwa sana kipaji ndani yake.
Ibrahim ajibu ukipenda muite “MIGOMBA” ukitaka pia unamweza mwita “MZEE WA MAKOLOKOLO” mwamba aliyetufanya tu enjoy soka na kuona ni mchezo raisi sana
Moyo wangu unaniuma sana najiuliza maswali yasiokuwa na jibu, najiuliza yupo wapi yule MZEE WA MAKOLOKOLO tuliyemzoea mbona haonekani kitambo hatupati tena zile raha za soka tulizopata zamani.
Ukipata nafasi ya kuonana nae popote alipo mwambieni hakuna mchezaji mzawa compete kwenye eneo la kiungo mshambuliaji kama yeye
popote utakapo mkuta ajibu katika mitaa, usisite mwambie kuwa maisha hayajawahi kuwa raisi ila apambane kama atabisha basi mpe kioo kisha mvalishe jezi ya yanga kisha mwambie tunamtaka ajibu kama Huyu.
Pia usisite mwabie ajibu kuwa kama alikubali kuridhika basi muda wa kuridhika umeisha na sasa ni muda wa mapambano Maana maisha ni kupambana na kupumzika ni kaburini.
0718431472
emmasolomon825@gmail.com



Post a Comment