Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mwamuzi wa Marekani, Tori Penso, ameandika historia kwa kuwa mwanamke wa pili kuchezesha mchezo wa Kombe la Dunia kwa wanaume, baada ya Mfaransa Stephanie Frappart kufanya hivyo katika fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kwenye mchezo kati ya Ujerumani na Costa Rica.
Penso (39) amesimamia mchezo wa Kundi A mzunguko wa pili kati ya South Africa dhidi ya Jamuhuri ya Czechia uliochezwa Atlanta, Marekani, na kumalizika kwa sare ya mabao 1-1, na kuandika historia ya katika michuano hiyo.
Penso si mgeni kwenye michezo mikubwa ya kimataifa, Mwaka 2023 aliingia kwenye rekodi kwa kuchezesha fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake kati ya Hispania na England, na sasa ameongeza historia nyingine kwa kuwa mwanamke wa pili kupewa jukumu la kuwa mwamuzi wa kati katika Kombe la Dunia la wanaume.
Uteuzi wake unaonekana kuwa sehemu ya juhudi za FIFA za kuongeza uwakilishi wa wanawake katika ngazi za juu za uamuzi wa mechi, huku Kombe la Dunia la 2026 likiendelea kushuhudia hatua mpya katika historia ya soka duniani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment