MWAKINYO ACHEZEA KICHAPO KWA "TKO"

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Bondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, amepoteza pambano lake la uzani wa middleweight baada ya kusimamishwa kwa TKO katika raundi ya tisa dhidi ya Michel Soro wa Ivory Coast na Ufaransa kwenye pambano la raundi 12 lililofanyika Abidjan, Ivory Coast , June 11, 2026.

Matokeo hayo yameongeza idadi ya vipigo vya Mwakinyo kwa njia ya KO/TKO katika rekodi yake ya ngumi za kulipwa, huku yakimaliza safari yake katika pambano ambalo lilikuwa na ushindani mkubwa tangu mwanzo, hili linakuwa pambano wa latatu kwa bondia huyo kupigwa kwa KO tangu alipo Anza kucheza ngumi za kulipwa.

Hata hivyo, matokeo hayo hayapaswi kutafsiriwa moja kwa moja kuwa kiwango cha Mwakinyo kimeshuka, Sababu kubwa ni ubora wa mpinzani aliyekutana naye pamoja na uzoefu mkubwa alionao katika ngumi za kulipwa.

Soro amefikisha mapambano 45, ambapo ameshinda mara 41, kati ya hayo 28 kwa KO/TKO, huku akipoteza mara mbili na kutoka sare mara mbili. Takwimu hizo zinaonyesha alikuwa akimkabili bondia mwenye uzoefu mkubwa wa mapambano ya kiwango cha juu na uwezo wa kumaliza pambano kabla ya kengele ya mwisho.

Kwa upande wa Mwakinyo, hili lilikuwa pambano lingine muhimu katika jitihada zake za kuendelea kujijenga kwenye jukwaa la kimataifa Ingawa matokeo hayakuwa upande wake, kukutana na bondia mwenye rekodi kama ya Soro kunatoa kipimo halisi cha ushindani uliokuwepo ndani ya ulingo.

Baada ya pambano hilo, macho ya wadau wa ngumi yataelekezwa kwenye hatua inayofuata ya Mwakinyo, huku wakisubiri kuona namna atakavyorejea ulingoni katika mapambano yajayo.

Rekodi ya Soro na historia yake ya ushindi wa mapema imeonyesha kuwa kushindwa kwa Mwakinyo kulitokana na ubora wa mpinzani aliyekuwa mbele yake, si matokeo yanayoweza kutumika peke yake kuamua kiwango chake cha sasa.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments