✍️ Emmanuel Masuza
Mwanakwetu Sports
Pale Iringa kuna historia kubwa sana iliyohifadhiwa kuhusu Chief Mkwawa ukipenda mwite “Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga” mwanaume shujaa aliyewatesa wajerumani zaidi ya Miongo kadhaa chini ya ngome yake ya Kalenga
Wajerumani waliona mwamba ana akili nyingi wakaamua kuchukua fuvu na kusepa nalo kwao ujerumani, historia hii inanifanya nimkumbuke kijana aliyekuwa akiendesha boda boda na kujitafutia riziki yake pale mitaa iringa ,jina lake anaitwa “CLEMENT MZIZE” moja ya vijina waliokuwa na ndoto kubwa ya kuwa Mchezaji nguri wa soka licha ya kuwa dereva boda boda kipindi hicho bado aliamini katika ndoto yake ya soka na alikuwa akijusisha na soka la mtaani wanangu wa pale keko makurumbasi wanaliita” NDONDO” Alikuwa maarufu sana kwa kucheza ndondo pale iringa waulize masela wa ILULA atakusimulia hadithi nzuri na tamu ya soka kutoka kwa kijana yule dereva toyo .
Kuna msimo wa wakikristo unasema wakati wa bwana ukifika hakuna wa kuzuia basi bwana wakati wa Mzize kwenda kuishi kipaji chake kilifika baada ya ujio wa aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga wakati huo MSINDO MSOLLO kutembelea iringa basi wazee wa mkoa ule wakamkabidhi Clement Mzize kama zawadi na kuondoka nae mpka Dar es Salaam na kujiunga na timu ya vijana ya Yanga ambapo alicheza kwa mafanikio makubwa mpka mwaka 2022 alipoaminiwa na kocha Nasreddine Na kupewa nafasi kucheza kikosi cha wakubwa ndani ya yanga
Hivi unaukumbuka usiku wa kihistoria katika uwanja wa Benjamin Mkapa, ambao ulifurika mashabiki, ulikuwa ni usiku wa mabadiliko makubwa. Jina la Clement Francis Mzize, staa kinda wa soka la Tanzania, liliingia katika vitabu vya historia ya soka la Afrika. Katika pambano la kundi A la mashindano ya TotalEnergies CHAN 2024, Mzize alifunga mabao mawili dhidi ya Madagascar na kuisaidia timu yake ya Taifa Stars kufuzu robo-fainali kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya michuano hiyo. Usiku huo, hakika, haukuwa tu usiku wa utendaji wa kawaida wa mpira, bali ulikuwa ni usiku wa ufunuo wa nyota mpya.
Huyu ndiye clement Mzize mtoto aliyetolewa kama zawadi na kuwa nyota mkubwa bongo.




Post a Comment