Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Mchezaji wa timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi kwa sasa ndiye mfungaji bora wa muda wote kwenye michuano ya kombe la Dunia baada ya kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa kundi J dhidi ya Austria na kufikisha Jumla ya mabao 18.
Awali, rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na mchezaji wa Ujerumani klose, ambaye anamabao 16 .katika msimamo wa wafungaji bora wa muda wote ushindani umeongezeka baada ya mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe kufikisha mabao 16 mabao mawiliI nyuma ya Lionel Messi.
Rekodi hii huenda ikavunjwa muda wowote kutokana na ushindani wa upachikaji mabao uliopo kati ya Messi na Mbappe , iwapo Mbappe atafanikiwa kuvunja historia hiyo basi itakuwa ni historia iliyo vunjwa mara mbili ndani ya makala Moja.
Mbali ya ushindani huo, wawili hao pia wapo kwenye vita ya kiatu Cha dhahabu ambapo kwenye michezo miwili tayali Messi ana mabao matano akifuatiwa na Mbappe ambaye anamabao manne sambamba na mshambuliaji wa Norway Erling Halaand.
Hivyo kwa Kasi hii ya upachikaji mabao huenda makala hii ya kombe la Dunia ikatoa mfungaji bora mwenye mabao mengi tofauti na makala zingine .
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com


Post a Comment