Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, ameendelea kuandika historia katika soka la dunia baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao katika mechi saba mfululizo za Kombe la Dunia.
Rekodi hiyo ilianza mwishoni mwa Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar, ambapo Messi alifunga katika michezo minne ya mwisho ya Argentina kuanzia hatua ya 16 bora hadi fainali. Msururu huo umeendelea katika Kombe la Dunia la 2026 baada ya kufunga katika mechi tatu za kwanza za Argentina.
Katika Kombe la Dunia la 2022, Messi alifunga dhidi ya Australia (hatua ya 16 bora), Uholanzi (robo fainali), Croatia (nusu fainali) na Ufaransa (fainali), akiongoza Argentina kutwaa ubingwa wa dunia kwa mara ya tatu katika historia ya taifa hilo.
Mwaka 2026, nyota huyo ameendelea kuzifumania nyavu katika kila moja ya mechi tatu za kwanza za Argentina za hatua ya makundi, hatua iliyomfanya kufikisha mechi saba mfululizo za Kombe la Dunia akiwa amefunga bao.
Rekodi hiyo inazidi kuimarisha kuwa Messi ni miongoni mwa wachezaji wenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya Kombe la Dunia, huku akiendelea kuongeza idadi ya mabao na mchango wake katika mashindano hayo makubwa ya soka duniani.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.


Post a Comment