Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Lionel Messi amefunga hat-trick yake ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia na kuiongoza Argentina kuifunga Algeria mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi J uliochezwa usiku wa kuamkia Leo June 17, 2026.
Messi amefunga mabao yote matatu ya Argentina na kuiwezesha timu hiyo kupata ushindi wake wa kwanza katika michuano hiyo, Mabao hayo pia yamemfikisha mshambuliaji huyo kufikisha mabao 16 kwenye Kombe la Dunia na kufikia rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Miroslav Klose wa Ujerumani kama mfungaji wa muda wote mpaka sasa.
Katika mchezo mwingine wa Kundi I, Ufaransa iliifunga Senegal mabao 3-1 huku Kylian Mbappe alifunga mabao mawili katika ushindi huo na kuongeza idadi ya mabao yake ya Kombe la Dunia kufikia mabao 14 kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote akiwa anashika nafasi ya nne.
Mbappe sasa anabaki mabao mawili kufikia rekodi ya mabao 16 inayoshikiliwa kwa pamoja na Messi na Klose wakati michuano ya Kombe la Dunia 2026 ikiendelea nchini Marekani, Canada na Mexico.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment