Madrid yagonga mwamba kwenye mbio za kusajili mastaa Ulaya

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Ndoto za Real Madrid kuendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili mastaa wa Ulaya zinaonekana kugonga mwamba baada ya kushindwa kupata baadhi ya wachezaji waliokuwa kwenye rada zao katika dirisha hili la usajili.

Mabingwa hao wa Hispania walitajwa kuonyesha nia ya kumhitaji kiungo wa Paris Saint-Germain, Vitinha pamoja na Joao Neves, lakini taarifa kutoka kwa wakala wao Jorge Mendes zimeweka wazi kuwa wawili hao hawataondoka ndani ya klabu hiyo ya Ufaransa.

Kupitia taarifa iliyotolewa, Mendes alisema Vitinha na Joao Neves ni sehemu muhimu ya mipango ya PSG na hawakuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaoweza kuuzwa kwenda Madrid au klabu nyingine yoyote.

Kauli hiyo imekuja ikiwa ni mwendelezo wa Madrid kukutana na ugumu katika majaribio yao ya kuwasajili mastaa mbalimbali kutoka klabu kubwa za Ulaya.

Awali, Bayern Munich ilikataa ofa inayodaiwa kufikia euro milioni 150 kutoka Real Madrid kwa ajili ya kumuuza Michael Olise, huku mabosi wa klabu hiyo wakionyesha kutokuwa tayari kuachana na mchezaji huyo.

Wakati huohuo, Madrid pia walikumbana na kikwazo katika harakati za kutafuta sajili ya Julian Alvarez baada ya rais wa klabu Enrique Cerezo kuweka wazi kuwa mshambuliaji huyo hakuwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa.

Kutokana na hali hiyo, Real Madrid sasa wanaendelea kusaka njia nyingine za kuongeza nguvu kikosini huku baadhi ya malengo yao makubwa ya kusajili majina makubwa yakionekana kufifia kufuatia misimamo ya klabu katika soko la usajili.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments