Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Azam FC imefuzu kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Yanga SC katika mchezo wa nusu fainali ya pili iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90 za kawaida, hali iliyolazimisha mchezo kuongezwa dakika 30 za nyongeza na Azam FC ikaanduka bao la ushindi katika muda wa nyongeza na kufuzu fainali kwa ushindi wa mabao 3-2.
Katika mchezo huo, mabao yote matano yalifungwa kwa njia ya kichwa tukio lililoifanya nusu fainali hiyo kuandika historia ya kipekee kwani haijawahi kutokea mchezo mmoja kutoa mabao matano yote kwa mtindo wa kichwa.
Kwa ushindi huo, Azam FC itakutana na Simba SC katika mchezo wa fainali ambapo Simba ilitinga hatua hiyo baada ya kuiondoa Coastal Union kwa ushindi wa mabao 4-0 katika nusu fainali ya kwanza iliyopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
klabu ya Yanga imeondolewa kwenye michuano hiyo ikiwa bingwa mtetezi wa taji hilo, ambalo ilikuwa imelinyakua mara nne mfululizo na rasmi wanavuliwa ubingwa na bingwa mpya wa mashindano hayo atapatikana mwanzoni mwa mwezi Julai ambapo utapigwa mchezo wa fainali.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com



Post a Comment