✍️ Emmanuel Masuza
Mwanakwetu Sports
Ilikuwa ni mei 31 mwaka 1987 kutoka unyamwezini tabora pale maskani ya chief mirambo alizaliwa haruna moshi ukipenda muite “BOBAN” fundi wa boli aliye funga ndoa na soka aliyeapa kuwapa burudani wanazi wa kambumbu, hakika Mwamba alikuwa na dunia yake ya soka wewe lipa mzunguko ama VIP mengine mwachie yeye
Mwaka 2004 wakati anaingia mitaa ya kariakoo yalipo maskani ya wekundu wa msimbazi simba akitokea moro United , simba ile iliyokuwa na majina ya kutisha kama vile ulimboka mwakingwe ‘VCD’ Suleiman matola, Joseph kaniki ‘golota’ shabaani kisiga ‘malobe’ haruna alipewa jezi namba kumi mgongoni kazi yake ilikuwa ni moja kupika, kuunganisha na kufunga tu, nyie mlioenda shule mnakumba kazi ya catalyst kwenye chemistry basi bwana mwamba haruna moshi ‘BOBAN’ alikuwa kichocheo cha Burundani za Simba. jukwaa gani pale uwanja wa taifa lilikuwa halinyanyuki na kushangilia pindi mwamba akishika mpira, zile pasi mnyoofu, usijali sana kuhusu Mtindo wa nywele zake, hakika mtoto wa chief mirambo alituonesha utamu wa soka
Haruna moshi ‘BOBAN’ mbali na kucheza simba amewahi kupita pia katika vilabu kama vile MORO UNITED, MBEYA CITY, COASTAL UNION, FRIENDS RANGERS, AFRICAN LYON, MUSCAT CLUB YA OMAN
Unataka useme Nini mpaka akapewa jina la mchawi mmoja ZVONMIR BOBAN, mwamba kutoka Croatia, mchawi wa kusambaza burudani pale SanSiro, waitaliano walikuwa wanamuita the Croatian Maestro, wabongo tukampa Haruna, zile field vision, ball control na set pieces specialist za ZVONMIR BOBAN, wahuni tukampa Haruna MOSHI wa TABORA
Kuna uhusiano gani Kati ya jina la Haruna na soka?? Kuna uhusiano gani Kati ya Haruna wa kisenyi na Haruna wa TABORA? Ni maswali yasiokuwa na majibu, tupeni four figure tusake hiyo ‘X’ Gefle IF kutoka Sweden wanakumbuka burudani za muhuni mstaarabu, wazungu waliona jamaa ataenda ligi kubwa Ulaya Ila haikuwa hivyo, Nini kilitokea anajua Haruna na Mungu wake
Huyu ndie Haruna Moshi Boban Bana



Post a Comment