LAMMENS SAJILI BORA EPL 2025/26

 

Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Golikipa wa Manchester United, Senne Lammens, ameibuka mshindi wa tuzo ya “Best Signing of the Season” katika Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2025/2026, hatua iliyoibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wachambuzi wa soka.

Lammens ambaye alijiunga na United akitokea klabu ya Royal Antwerp, alicheza michezo 32 ya EPL msimu huu akiwa na clean sheet nane huku akiokoa mipira 79 katika kipindi chote cha msimu.

Lammens, amepiga Jumla ya pasi 941 huku asilimia 59% ya passi hizo zikiwa ni sahihi, kwa upande wa pasi ndefu kapiga 571 huku asilimia 34% zikiwa sahihi, kwa upande wa nidhamu hajaonyeshwa kadi yote kwenye msimu mzma.

Mchango wake umeisaidia United kumaliza nafasi ya tatu na kufuzu kucheza mashindano ya UEFA kwa msimu ujao.

 Majina mengine yaliyokuwa yakitajwa kupewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo hiyo ni pamoja na Rayan Cherki wa Manchester City, Viktor Gyokeres pamoja na Dominic Calvert-Lewin kutokana na mchango wao mkubwa wa mabao na ubunifu ndani ya timu zao.



Hata hivyo, EPL ilieleza kuwa tathmini ya tuzo hiyo ilizingatia mchango wa jumla wa mchezaji, uthabiti pamoja na athari yake kwa mafanikio ya timu katika msimu mzima.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.


0/Post a Comment/Comments