Kwaku: "Cape Verde wataiondosha Argentina , Nimeliona tayari"


Timothy Lugembe,

Mwanakwetusports.

Mganga wa jadi kutoka Ghana, Nana Kwaku Bonsam, amezua mjadala baada ya kudai kuwa Timu ya Taifa ya Cape Verde itaiondoa Argentina katika hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia 2026.

Bonsam, ambaye aliwahi kuvuta hisia za wanasoka baada ya kutabiri kuwa mshambuliaji wa England, Harry Kane, hatafunga katika mchezo dhidi ya Ghana, sasa ametoa utabiri mwingine unaolenga moja ya mechi zinazosubiriwa kwa hamu kwenye hatua ya mtoano.

Kupitia kauli yake, mganga huyo alisema: "Cape Verde will eliminate Argentina. I have seen it already," akimaanisha kuwa tayari ameona Cape Verde ikiiondoa Argentina kwenye mashindano hayo.

Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa soka, huku wengi wakilinganisha ukubwa wa Argentina kwenye soka la dunia na safari ya Cape Verde, ambayo imeandika historia kwa kufuzu hatua ya 32 bora kwa mara ya kwanza.

Ingawa utabiri huo unaonekana kuwa mgumu kutimia kutokana na historia na rekodi ya Argentina katika Kombe la Dunia, mpira wa miguu umeendelea kuthibitisha kuwa matokeo huamuliwa ndani ya dakika 90 za mchezo.

Cape Verde na Argentina zinatarajiwa kukutana July 4, 2026, katika hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia. Sasa macho ya mashabiki yataelekezwa kwenye mchezo huo kusubiri kuona kama utabiri wa Nana Kwaku Bonsam utatimia au utaishia kuwa sehemu ya mjadala pekee.

0767915473,

lugembetimothy01@gmail.com.



0/Post a Comment/Comments