Timothy Lugembe,
Mwanakwetusports.
Michuano ya Kombe la Dunia 2026 imeanza kuonyesha dalili za ushindani kupitia michezo ya kirafiki inayochezwa na mataifa mbalimbali kuelekea mashindano hayo yatakayofanyika nchini Marekani, Canada na Mexico.
Baadhi ya timu zinazotajwa kuwa na nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo zimeanza kupata matokeo yasiyotarajiwa katika maandalizi yao, jambo linaloonyesha kuwa ushindani unaweza kuwa mkubwa zaidi kuliko ilivyotarajiwa.
Ugumu wa mashindano umepimwa kupitia michezo miwili iliyo husisha timu mbili zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo, timu hizo ni France na Spain , timu ambazo kwa sasa ni bora Dunia zinazo undwa na wachezaji wenye vipaji na uzoefu mkubwa.
kupitia mchezo wa kirafiki kati ya France dhidi ya Ivory coast , timu ya taifa ya Ufaransa ilikubali kupoteza mabao 2-1 . Matokeo hayo sio kwa bahati mbaya bali mbinu na umakini viliamua matokeo ya mchezo kwani Kila timu ilianzisha kikosi kamili ambacho kwa asilimia kubwa ndicho kitatumika wakati wa mashindano.
Wakati huo huo, Hispania nayo ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Iraq katika mchezo mwingine wa maandalizi kuelekea michuano hiyo, na kuacha maswali mazito kuhusu mustakabali mzima wa timu kubwa kuelea mashindano.
Kwa mujibu wa viwango vya FIFA, Ufaransa ipo nafasi ya kwanza duniani huku Ivory Coast ikishika nafasi ya 34. Hispania ipo nafasi ya pili wakati Iraq ikishika nafasi ya 57.
Tofauti hiyo ya viwango haikuonekana wazi ndani ya uwanja, hali inayozidi kuonyesha kuwa mataifa mengi yanaendelea kujiandaa kwa kiwango cha ushindani mkubwa.
Matokeo hayo yanaendelea kutoa picha kwamba Kombe la Dunia 2026 linaweza kuwa na ushindani mkubwa pamoja na uwezekano wa kushuhudiwa matokeo ya kushangaza kutoka kwa timu ambazo hazipewi nafasi kubwa kabla ya mashindano kuanza.
0767915473,
lugembetimothy01@gmail.com.



Post a Comment